Kuhusu sisi

Karibu Dalali Digital Agency, jukwaa la kidijitali linaloboresha sekta ya mali isiyohamishika hapa Tanzania.

Sisi ni suluhisho la kipekee kwa wanunuzi na madalali wa mali kwa lengo la kurahisisha na kuharakisha mchakato wa kuuza, kununua, na kukodisha mali.

Katika Dalali Digital, tunawawezesha madalali kujisajili na kutangaza mali zao moja kwa moja kwenye tovuti yetu. Hivyo wanunuzi wanaweza kutembelea jukwaa letu na kuona orodha ya mali mbalimbali, kuanzia nyumba, viwanja, maghala, hadi majengo ya kibiashara.

Vigezo na Masharti

1. Usajili:

Madalali wanapaswa kujisajili kwa kutoa taarifa sahihi ili kuweza kutumia huduma za jukwaa letu.

2. Uhalali wa Mali:

Madalali wanawajibika kuhakikisha kwamba mali wanazoposti ni halali na zina nyaraka sahihi.

3. Faragha:

Tunaheshimu taarifa za watumiaji wetu na tutahifadhi data zao kwa mujibu wa sera yetu ya faragha.

4. Matumizi ya Jukwaa:

Watumiaji wanatakiwa kutumia jukwaa letu kwa njia halali bila kudhuru haki za wengine.

5. Uwajibikaji:

Dalali Digital Agency si mdhamini wa ubora au uhalali wa mali zilizopostiwa; tunatoa tu jukwaa la kuwasiliana.

Kwa maoni, msaada, au maswali, tafadhali wasiliana nasi kupitia habel@dalali.digital au WhatsApp namba 0693690480

Nyumba
Viwanja
Fremu
Mashamba